novenaaaa
NOVENA YA MT RITA Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina. Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa pumziko, huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu, najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Rita, unayeng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za Kanisa Katoliki, natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini, kwa hamu nangojea, kupata kile nikiombacho {hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita}. Nifikishie ombi langu kwa Yesu wa msalaba. Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopitia majaribu, kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa, uliyomtolea M...