Posts

Showing posts from March, 2020

novenaaaa

NOVENA YA MT RITA  Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Amina. Natazama huku na huko bila ya kupata mahali pa pumziko, huku macho yangu yakiwa yametiwa uvuli kwa uchungu. Matarajio yoyote ya dunia hii hayauchangamshi moyo wangu unaosononeka kwa uchungu, najiona nimepotea kabisa. Lakini wewe kipenzi Mtakatifu Rita, unayeng’ara kama nyota inayoangaza kwa mwanga usio kifani katika nguvu na nguzo za Kanisa Katoliki, natambua wewe unaimulika njia yangu yenye giza na unaupa shime moyo wangu unaoomboleza kwa uchungu. Ninakuamini, kwa hamu nangojea, kupata kile nikiombacho {hapa omba hitaji lako unalotaka kumwomba Mungu kupitia Mtakatifu Rita}. Nifikishie ombi langu kwa Yesu wa msalaba. Nakumbuka kipindi kile kigumu kwako wakati moyo wako ulipopitia majaribu, kwa utii ulipokubali kufunga ndoa na mtu ambaye alikutesa hata kutishia maisha yako. Hata hivyo ulimpenda sana na alipofariki uliomboleza kifo chake kwa huzuni kuu. Kwa sadaka yako ya kishujaa, uliyomtolea M...

MAANA KAMILI YA KWARESMA

Maana kamili ya Kwaresma Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu. Kwaresma ni kipindi maalum ambacho wakristo wanakumbuka maisha ya Yesu kristo hapa duniani hususan mateso, kufa na kufufuka kwake. Ni kipindi cha kutafakari maana na umuhimu wa dhabihu ya YESU kristo katika ukombozi wa dunia na kumrudia Mungu. Aidha ni kipindi ambacho wakristo wanakumbushwa kufanya toba na kumrudia Mungu kwa mujibu wa maandiko matakatifu. Ingawa kipindi cha kwaresma ni kipindi cha mafungo kwa wakristo, watu wengi na hasa wa dini nyingine hushindwa kutambua funga inayofanywa na wakristo katika kipindi hiki na hasa kwa sababu wakristo wengi huonekana wakiendelea kula na kunywa wakati wa kwaresma. Wakristo walio wengi p...

SARA YA JIONI

TUNAKUSHUKURU, EE MUNGU KWA MAPAJI YOTE ULIYOTUJALIA LEO AMINA BABA YETU……………….. SALAMU MARIA………………. SALA YA IMANI…….YA MATUMAINI………YA MAPENDO SALA YA KUTUBU TUWAZE KATIKA MOYO WETU MAKOSA YA LEO TULIYOMKOSEA MUNGU KWA MAWAZO,KWA MANENO, KWA VITENDO NA KWA KUTOTIMIZA WAJIBU (HUSUBIRI KIDOGO) NAKUUNGAMIA MUNGU MWENYEZI,NANYI NDUGU ZANGU,KWANI NIMEKOSA MNO KWA MAWAZO,KWA MANENO,KWA VITENDO NA KWA KUTOTIMIZA WAJIBU,NIMEKOSA MIMI,NIMEKOSA SANA.NDIYO MAANA NAKUOMBA MARIA MWENYE HERI,BIKIRA DAIMA,MALAIKA NA WATAKATIFU WOTE,NANYI NDUGU ZANGU,MNIOMBEENI KWA BWANA MUNGU WETU. MUMNU MWENYEZI ATUHURUMIE ATUSAMEHE DHAMBI ZETU,ATUFIKISHE KWENYE UZIMA WA MILELE.AMINA SALA YA KUOMBEA WATU…………………… KUSIFU……………………

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TISA

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA TISA, JUMAMOSI BAADA YA PASAKA Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa. Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini: Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee roho za WALE WALIOKWISHAINGIA HALI YA UVUGUVUGU, na uwazamishe katika kilindi cha Huruma yangu. Roho hizi huumiza sana Moyo wangu. Roho yangu iliteseka sana kwa kinyaa cha kutisha kule bustanini kwa sababu ya roho hizi vuguvugu. Ni wao waliosababisha nilie; Baba ikiwa ni mapenzi yako uniondolee mbali kikombe hiki nisikinywe. Kwa watu hawa, tumaini la mwisho lililowabakia ni kuikimbilia Huruma yangu tu basi”. Kiongozi: Tuwaombee watu walio na hali ya uvuguvugu, hali ya hatari kwa wokovu, ambao walisababisha mateso makali sana kwa Yesu Kristu kule bustanini mwa mizeituni. Wote: Ee Yesu mwenye Huruma...

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA NANE

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA NANE, IJUMAA BAADA YA PASAKA Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa. Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini: Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee roho za wale WALIOFUNGWA BADO TOHARANI, na uwazamishe ndani ya Bahari Kuu ya Huruma yangu. Humo, mafuriko ya Damu yangu, yazimishe miali ya motto mkubwa unaowachoma. Roho hizi zote hupendwa sana nami. Wako humo toharani kwa ajili ya kulipia Haki yangu waliyoikosa hapa duniani. Wewe una uwezo wa kuwapatia faraja. Chota rehema zote za Kanisa langu na uzitolee kwa ajili yao. Ungalijua tu ukali wa mateso yao, loo! Ungetolea daima sadaka za kiroho kwa ajili yao, na kulipa deni zima la Haki ya Mungu”. Kiongozi: Tuwaombee marehemu wa toharani, wanaoilipia Haki ya Mungu, ili mtiririko wa Huruma wa Damu ya Yes...

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA SABA

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA SABA, ALHAMISI BAADA YA PASAKA Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa. Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini: Maneno ya Mwokozi: “Leo niletee roho za wale AMBAO KWA NAMNA YA PEKEE HUIHESHIMU NA KUITUKUZA HURUMA YANGU, na uwazamishe ndani ya Huruma Yangu. Roho hizi ndizo zilizonisikitikia zaidi wakati wa mateso yangu na kuipenya kabisa roho yangu. Hawa ndio vielelezo na sura halisi ya Moyo wangu wenye Huruma na Wema. Roho hizi zitakuja kung’aa kwa namna ya pekee katika maisha ya milele ijayo. Hakuna hata mmoja kati yao atakayetupwa katika moto wa milele. Mimi Mwenyewe nitamkinga kwa namna ya pekee kila mmoja wao saa ile ya kufa kwao. Kiongozi: Tuziombee roho za wale wanaoiheshimu kwa namna ya pekee Huruma ya Mungu, na kwa njia hii huwa sur...

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA SITA

NOVENA YA HURUMA YA MUNGU SIKU YA SITA, JUMATANO BAADA YA PASAKA Novena hii pia inaweza kusaliwa wakati wowote na katika kipindi chochote cha mwaka lakini inapendekezwa Novena ianzwe katika siku ya Ijumaa. Tujiandae kusali kwa kuanza na sala za awali kama vile Uje Roho Mtakatifu pamoja na Sala ya kutubu kisha tuendelee kama inavyoonyeshwa hapa chini: Maneno ya Mwokozi wetu: “Leo niletee roho za WATU WALIO WAPOLE NA WANYENYEKEVU WA MOYO, PAMOJA NA ROHO ZA WATOTO WADOGO, na uzizamishe katika kilindi cha Huruma yangu. Roho hizi hufanana kwa ukaribu zaidi na Moyo wangu. Watu hawa ndio walionitia nguvu wakati wa mateso na uchungu wa mahututi yangu. Niliwaona kama malaika wa duniani, ambao watakesha daima kuabudu katika altare zangu. Kwa mafuriko yangu, nitawamwagia neema zangu zote, kwa maana ni roho ile tu iliyo na unyenyekevu inaweza kupata neema zangu. Ninawapendelea watu walio wanyenyekevu na kuwaamini sana.” Kiongozi: Tuwaombee watoto wadogo pamoja na roho zile zenye unyofu ka...